Na Angess Francis, Globu ya jamii
BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA)limesema kuendele kutoa ushirikiano kwa wasanii wa nyanja mbali mbali hapa nchini ili wafikie mafanikio yao.
Ambapo leo BASATA jijini Dar es Salaam limepokea zawadi ya shukurani kutoka kwa Miss Teen Heritage international 2016 Cesilya Godfrey ambaye ameambatana na uwongozi wake wa kampuni ya See The African Link.
Mrembo huyo amekabidhi Cheti cha kuonyesha fadhila kwa kile alichosaidiwa.Mashindano hayo yalifanyika nchini Sri Lanka na kuwashirikisha washirki 15 wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 18 kutoka nchi mbalimbali duniani.Akizungumza leo akiwa BASATA ,Mrembo huyo amesema alishika nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikienda kwa raia kutoka Zimbabwe.
Amesema kuwa BASATA ndio waliofanikishia yeye kushiriki kwa kumpa vibali vya kutafuta Wadhamini wa kumpeleka katika mashindano hayo."Niliona matangazo kwenye mitandao kuwa wanatafutwa washiriki wa kushindania Taji hilo,nikavutiwa ndio nikaandika maombi nikakubaliwa,baada ya hapo nikaanza mchakato wa kutafuta wadhamini huku nikisaidiwa na BASATA"amesema.
Mkurugenzi wa BASATA Godfrey Mngereza amesema walikuwa wako bega kwa bega na mrimbwende huyo tangu mwanzo kwa kuanza na kumtambulisha kwa wadhamini ili kufanikisha ndoto zake."Hii ni kuonesha pia Baraza lipo karibu sana na wasanii wa sanaa mbalimbali pamoja na wadau katika kuunga mkono na kutia sapoti kazi zao ili kufanikisha ndoto zao".Amesema Mngereza.
Pia Mngereza amempongeza Cecilya kwa kufanikiwa kupeperusha bendera ya nchi kimataifa kwa kufanya vizuri na kunyakua nafasi ya pili.Wakati huo huo Meneja wake Zuberi Mohamed 'Niva' ambaye ni msanii wa Bongo Muvi amesema imekuwa ni faraja kwa nchi kwa mrembo huyo kutangaza utaifa wetu katika nchi zingine mbalimbali.
Mkurungenzi mkuu Baraza la Sanaa Taifa Godfrey Mngereza akipokea Zawadi ya cheti cha shukurani leo ofisini kwake (BASATA) Jijini Dar es Salaam kutoka kwa uongozi mzima wa Kampuni ya See The African Link,ambao ndio kwa sasa unamsimamia kazi za Miss Teen Heritage International 2016 Cecilya Godfrey.
Picha ya Pamoja Mkurugenzi mkuu Baraza la Sanaa Taifa Godfrey Mngereza wa pili kushoto,Meneja wa Miss Teen Heritage international 2016 Zuberi Mohamed (NOVA) kushoto,Miss Tee Heritage International Cecilya Godfrey wa pili kutoka kilia, Meneja wa see the African Link Irene Mitema wa kulia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...