Mwanza, ‘The Rock City’ kama inavyofahamika kwa wengi nchini Tanzania, leo imeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa huduma ya usafiri kidijitali jijini humo. 

Mwanza, Taxify, ambayo ni miongoni mwa Kampuni kubwa zinazotoa huduma ya usafiri kidijitali barani Ulaya na Afrika imezindua rasmi huduma zake jijini Mwanza huku mamia ya madereva wakiwa tayari wamesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo yote ya jiji.

Katika kusherekea uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify inatoa punguzo la asilimia 50 kwa abiria kuanzia tarehe 28 Mei, 2018 mpaka mwisho wa mwezi wa sita mwaka huu. Gharama za usafiri kwa kipindi hiki ni:- Kuanza safari ni TZS 700, Kwa kilometa ni TZS 460, Kwa dakika ni TZS 70 huku gharama ya chini kabisa ya safari ikiwa ni TZS 2,000.

“Mwanza ni jiji lenye watu zaidi ya milioni 3.5, barabara nzuri zenye ubora, Huduma bora ya mitandao inayopatikana kirahisi na maelfu ya magari. Tulifanikiwa kupokea maombi mengi kutoka kwa wakazi wa jiji hili waliokuwa na shauku ya kutumia huduma yetu lakini huduma yetu ilikuwa bado haijafika jijini hapa, jambo hili limetusukuma kuzindua rasmi huduma yetu leo jijini hapa. 

Mamia ya madereva wameshasajiliwa kwenye jukwaa letu na tayari tumeshaona mamia ya safari ambazo zimefanyika hata kabla ya uzinduzi rasmi. Mwanza ipo tayari kwa huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao na tunaimani kuwa huduma hii itafanya vizuri katika jiji la ‘Rock City’ alisema Remmy Eseka, Mkuu wa Operesheni, Taxify Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyozinduliwa hivi karibuni jijini humo. Jiji la Mwanza sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji (kushoto) akikabidhi fulana kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Ms. Mary Tesha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo sasa limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Kampuni ya Taxify inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
Meneja Uendeshaji wa Taxify nchini Tanzania, Remmy Eseka akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
Meneja wa Taxify Kanda ya Ziwa, Milumbilwa Kipimo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hafla ya uzinduzi ya huduma ya Taxify hivi karibuni jijini Mwanza. Jiji hilo limeingia kwenye ligi ya miji ya kisasa duniani baada ya kuingia rasmi kwa Taxify, Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kidijitali.
Msanii wa muziki wa hiphop, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...