Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony
Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri
kwa mafanikio makubwa aliyopata kupitia kilimo cha mbogamboga.
Aidha
amempongeza kwa kuajiri takriban Wafanyakazi 236 sambamba na
uanzishwaji wa mpango wa ushikirishwaji wakulima wadogo
wadogo(out-growers) ambao wataiuzia Kampuni hiyo mazao mbalimbali ya
mboga mboga ili aweze kufikia mahitaji ya soko la nje ambayo ni tani 26
kwa wiki za maharage machanga na njegere changa.
Mavunde
ametoa pongezi hizo leo alipofanya ziara fupi kutembelea Mashamba hayo
ya Mboga mboga yaliyopo Kijiji cha Kiwele, Halmashauri ya Iringa
Vijijini yanayomilikiwa na Bi Hadija Jabiri kijana mdogo mwenye umri wa
miaka 27.
Mavunde
amesisitiza pia utekelezwaji wa agizo la Waziri Mkuu kwa Tawala za
mikoa juu ya utengwaji wa maeneo mahsusi kwa ajili ya shughuli za
kiuchumi za Vijana ili Vijana wengi zaidi wapate fursa za maeneo ya
kufanyia shughuli mbalimbali na pia kuitaka Mifuko ya Uwezeshwaji
Wananchi Kiuchumi kusaidia jitihada hizi za Bi Hadija ili aweze kufikia
mahitaji ya soko.
Akitoa
taarifa kwa Naibu Waziri Mavunde,Meneja wa PackHouse Bw.Ferdinand
Sinkala amesema kwamba Kampuni yao ina soko kubwa la Maharage na Njegere
changa katika nchi za Uingereza,Ireland na Sweden lakini changamoto
kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa ardhi ili kuwa na eneo kubwa zaidi
waweze kulima na kukidhi mahitaji ya soko la nje.
Amesema
kwa sasa wameamua kuwashirikisha wakulima wadogo wadogo kulima mazao
hayo ili waweze kukidhi mahitaji ya soko la tani 26 kwa wiki,lakini pia
ameiomba Serikali kuunga mkono jitihada za Vijana walioamua kushiriki
katika Kilimo hasa kilimo cha mboga mboga kwa kuwawezesha ili waweze
kufikia malengo yao.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikagua shamba la mboga mboga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikabidhiwa mboga mboga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwasikiliza wataalam wa GBRI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwa ameshika maharage machanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...