Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
NAIBU Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdalah Ulega ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa madaraja matatu wilayani Mkuranga mkoani Pwani
Akizungumzia ujenzi wa madaraja hayo ,Ulega ameeleza madaraja hayo matatu yatajengwa katika vijiji vitatu ambavyo ni Tamabani Mwanabilatu, na Kifaurongo.
Amesema ujenzi wa madaraja hayo hadi kukamilika kwake Julai mwaka huu utagharimu kiasi cha takribani Sh.bilioni 1.5.Aidha Ulega amemuagiza mkandarasi anayejenga madaraja hayo asichukue vibarua wa kutoka sehemu nyingine bali wachukuliwe katika vijiji ambavyo mradi huo wa ujenzi wa madaraja unafanyika ili wakazi wa maeneo hayo wapate vipato.
Pia Ulega amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kushirikiana na wakandarasi wa ujenzi ili kuweza kurahisisha kazi hiyo na kufanya mradi huo kuisha kwa wakati.Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARULA) Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Emmanuel Mubofu amesema miradi hiyo ita kamilika ndani ya miezi miwili tu, yaani kuanzia mwezi Mei hadi Julai mwaka huu.
Mubofu ameeleza mradi huo umeanza na kufikia Agosti wananchi wataanza kutumia madaraja hayo licha ya kuikamilisha Julai.Kuhusu fedha za ujenzi Mubofu ameeleza kuwa zimetoka mfuko wa barabara kwa ajili ya kero hizo za kimiundombinu zilizokuwa zinawakabili wakazi hao.
Aidha ameeleza wakandarasi wawili wameshaanza kazi na kwa asilimia 20 tayari ujenzi umekamilika.
Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega (watatu kutoka kulia) akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5
Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wanaichi wa kijiji cha Kifaurongo kabla katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akimsikiliza Kaimu Mejeneja Tarula Mkuranga Muhandisi Emmanuel Mubofu alienyosha mkono alipo tembelea mradi wa ujenzi wa madaraja.
Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na viongozi wa (CCM) wa Wilaya Mkuranga wakivuka Mto Mzinga.
Wananichi wa kijiji cha Kifaurongo wakivuka Mto Mzinga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...