Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
RAIS Dkt. John Magufuli leo Mei 7 ametembelea Chuo kikuu cha kilimo (SUA) katika kuhitimisha ziara yake akitokea mkoani Morogoro huku akielezea kufurahishwa na utendaji wa chuo hicho hasa katika kilimo ambacho kinategemewa na watanzania kwa zaidi ya asilimia 70.
Dk.Magufuli amesema hayo leo mkoani Morogoro ambapo amefafanua chuo hicho ni muhimu katika masuala ya viwanda kwani rasilimali zinazotegemewa zinazalishwa chuoni hapo.Rais amewaomba wanafunzi hao wasigeuze vyuo kama eneo la kufanya siasa bali wafanye kilichowaleta hasa kusoma na kufanya tafiti (research) na amewataka kutoingia katika mikumbo bali waangalie walikotoka na kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yo.
Pia ameeleza kuwa Chuo chochote kitakachofanya fujo kama Rais atawafukuza na haitafahamika lini watarejea vyuoni.Aidha ameeleza Serikali ipo kwa lengo la kuwasaidia ili kutimiza malengo yao.Katika ziara hiyo Dk.Magufuli ametoa Sh.bilioni 2 zilizotengwa kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ili kujenga mabweni katika chuo hicho na matrekta 10 kwa ajili ya uendeshaji wa chuo hicho.
Rais amesema kuwa chuo hicho tegemezi kimetengewa bajeti kubwa ya kimaendeleo kiasi cha Sh.bilioni 8 na amewasisitiza watendaji kutumia fedha hizo kwa uangalifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...