Na  Emmanuel  Massaka wa Globu ya jamii,Mkuranga

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imepiga marufuku  wakazi wa Wilaya hiyo na wanafunzi kutovuka katika mito,na badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji ikiwamo kuumizwa na wanyama katika mito hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Filbeto Sanga,katika kikao cha robo mwaka cha Baraza la madiwani  wilayani hapo."Kutokana na mvua kunyesha katika kipindi cha mwezi wa nne  na mwezi huu,miundombinu imeharibika na watu wamekuwa wakitumia mito kuvuka kwenda Shule na wengine kwenda kutafuta mahitaji.

" Sasa naomba wanafunzi na wananchi,wasitumie mito kuvuka kwani kuna baadhi ya watu walipoteza maisha pia kuna wanyama wakati katika mito hiyo," amesema.Amesema wanafunzi watano walipoteza maisha katika mvua na kuna watu makubwa ambao wamepoteza maisha,lakini wanawafuatilia ili baraza lijalo idadi yake itajulikana na kuambiwa walipoteza maisha.

Amesema kutokana na mvua kunyesha miundombinu imeharibika na baadhi ya kaya nyumbani zao zimejaa maji na  hari hiyo ilisababisha kuyahama makazi.Wakati huo huo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Juma Abeid amesema  halmashauri hiyo imefanikiwa kupata hati safi kutokana na kusimamia  vizuri miradi ya maendeleo ambayo imekamilika kwa wakati.

Akizungumza katika baraza la madiwani alisema kuwa,Serikali kila mwaka wanafanya ukaguzi katika halmashauri zote nchini na kama halmashauri itakuwa haikufanya vizuri inapata hati chafu.Amesema kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wakuu wa idara na madiwani,wameweza kufanya kazi kwa pamoja na kufanikisha fedha za miradi ya maendeleo kutumika kama ilivyokusudiwa,kukaa vikao kwa wakati na kusimamia fedha vizuri za halmashauri.

"Yote hayo tumeyafanya kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani na tukafanikiwa kupata hati safi," amesema Juma Abeid.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Dk Stephen Mwandambo (wapili kutoka kushoto) akiwa na watendaji wa wilaya hiyo katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la Madiwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga akizungumza Michuzi juu ya kupiga marufuku kwa wananchi na wanafunzi kutokuvuka mito badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji na  kuumizwa na wanyama katika mito hiyo (kushoto)  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la madiwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...