Na Ally Ruambo, Kilwa Masoko
Wakulima wa zao la ufuta Wilayani Kilwa wameipongeza Halmashauri ya Wilaya Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla kwa kuanzisha mfumo mpya wa Mnada katika ununuzi wa zao hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Wakulima, Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Kibaoni Amcos kutoka katika kijiji cha Zinga Kibaoni Bw. Adam Chumi amesema wamefurahishwa sana na uamuzi wa Halmashauri na Mkoa wa kuanzisha  mfumo wa Mnada.
Adam amesema mifumo ambayo ilikua inatumika katika ununuzi Ufuta ilikuwa inawakandamiza  sana na haikuwa na tija kwao hali ambayo ilikuwa inawakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo cha ufuta.
”Tunaishukuru sana Halmashauri yetu kwa kuunga Mkono wazo la kutumia Mfumo wa mnada katika uuzaji wa ufuta kwa sababu lina tija kwetu sisi kama wakulima.
Kwa miaka yote ambayo tumekuwa tunalima ufuta hatujawahi kuuza kilo ikazidi Shilingi 2000 lakini kama mlivyoona pale kwenye Mnada kuwa Ufuta utanunuliwa kwa Shilingi 2815 kwa Kilo jambo ambalo tulikuwa tunaliota miaka mingi.
Mwaka jana mimi na wenzangu wachache tuligoma kuuza Ufuta wetu kwa Shilingi 1650 kwa Kilo, tulikaa nao sana mwishoni tukauza kwa Shilingi 1850 kwa Kilo sasa unaweza kuona mwenyewe mabadiliko yaliyoletwa na huu mfumo”. Alisema Adam
Aidha Adam ameupongeza mfumo kwa jinsi unavyo fanya malipo ambao mkulima anaingiziwa pesa katika akaunti yake  baada ya mnada.
“Awali Mfanyabiashara alikua anakulipa fedha tasilimu mkononi jambo ambalo kwa usalama halikuwa zuri lakini pia wengi wao walikua wanakuja na Mizani ambazo zimechezewa swala ambalo lilikua linaongeza unyonyaji kwa mkulima” aliongeza Adam
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Zablon Bugingo amewataka Wakulima kutumia fedha zao kwa nidhamu ili ziweze kuwasaidia kiuboresha maisha yao  na kuwakumbusha kuweka akiba kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao
“Niwashauri tu kuwa fedha ambazo tutazipata msizifuje, zitumieni kwa nidhamu ya hali ya juu na mkubuke pia kuna msimu mwingine ambao nao unahitaji maandalizi ya mapema, Sitarajii kusikia kuna mkulima ametumia pesa zote akakosa hata pesa ya akiba ambayo itamuwezesha kuanzisha tena kilimo msimu ujao” alisema Bugingo.
Mnada wa uuzaji wa Ufuta katika kijiji cha Zinga Kibaoni wilayani Kilwa ni miongoni mwa Miradi iliyozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018.
C:\Users\RUAMBO\Desktop\IMG_20180625_135011_481.JPG
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Bw. Charles Kabeho akifungua Bahasha za Barua za maombi kujua kampuni iliyoshinda kununua Ufuta Wilayani Kilwa. (Picha :Ally Ruambo)
C:\Users\RUAMBO\Desktop\DSC00079.JPG
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Bw. Charles Kabeho (Kushoto) akizungumza na Wananchi wakati wa uzinduizi wa Mradi wa uuzaji wa zao la Ufuta kwa njia ya Mnada Wilayani Kilwa, Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai (Picha:Ally Ruambo) 
C:\Users\RUAMBO\Desktop\DSC00070.JPG
Sanduku la Chuma lilotumika kuhifadhia Barua za Maombi ya Kampuni mbalimbali ya Kununua Ufuta Wilayani Kilwa (Picha: Ally Ruambo)
C:\Users\RUAMBO\Desktop\DSC00062.JPG ufuta ukiwa tayari kwa mnada katika moja ya vyumba vya kuhifadhia ufuta katika Kjiji cha Zinga Kibaoni (Picha: Ally Ruambo)
C:\Users\RUAMBO\Desktop\bugingo edited.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa akifurahi na Wananchi katika uzinduzi wa Mradi wa Uuzaji ufuta kwa njia ya Mnada wilayani Kilwa katika Kijiji cha Zinga Kibaoni (Picha na Ally Ruambo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...