VICTOR  MASANGU, KIBAHA
MKUU  wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama  ametoa muda wa mwezi mmoja  kwa madereva wote wa pikipiki  kuhakikisha wanakuwa na leseni kwa lengo la kuweza kupunguza na kuondokana na  ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya watu na nguvu kazi ya Taifa hususani kwa  vijana hao.

Agizo hilo amelitoa  leo wakati wa mkutano maalumu ambao aliuandaa kwa lengo la kuweza kuwakutanisha na wadau mbalimbali  wa maendeleo ili kuweza kusikiliza kero pamoja na kubaini changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika utekelezaji wa  majukumu yao ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Pia  katika hatua nyngine Mkuu huyo alibainisha kuwa  vijana wengine  ambao ni madereva  wa pikipiki katika Wilaya Kibaha wamekuwa wakivunja sheria mbalimbali za barabarani ikiwemo kutokuwa na leseni  hivyo wanahatarisha usalama wa maisha yao pamoja na abiria ambao wanaowapakia kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na sheria za taratibu za usalama barabarani.

“Kwa kweli kutokana na kuwepo kwa changamoto hii ya madereva wa pikipiki nimeamua kuitisha mkutano kwa ajili ya kuwakutanisha wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na taasisi mbali mbali ili kuwez kujadili kwa pamoja na kuweza kuona namna gani tunaweza kuwasaidia vijana hawa waweze kupata leseni pamoja na kuwezeshwa katika mikopo,”alisema Assumpter.

Nao madereva  hao wa pikipiki wakizungumza katika mkutano huo wamesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kutokuwa na leseni, kofia ngumu pamoja na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala mbalimbali ya sheria za usalama barabarani hivyo kupelekea kusababisha kutokea kwa ajali ambazo zinapoteza  maisha ya watu pamoja na majeruhi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kufungua mkutano wa madereva wa pikipiki  kwa ajili ya kukutana na wadau kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo kutokuwa na leseni, pamoja na kofia ngumu ili kuweka mikakati ya kuwasaidia pamoja na kupunguza wimbi la ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza.
 Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kibaha Edward Gontako akizungumza na wanahabari kuhusina na mikakati waliyojiwekea katika kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikipelekea kupoteza maisha ya watu(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...