Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akipokea
salaam ya heshima kutoka kwa gadi maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake ikiundwa
na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) akikagua
gadi ya heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake alipofanya ziara ya kikazi katika
Jeshi la Magereza leo Julai 11,2018 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb)
akisalimiana na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada
ya kukagua gwaride maalum. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt.
Juma Malewa na aliyeshikanaye mkono ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza Musa Kaswaka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola (Mb) (katikati)
katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza
wakiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo kabla ya kuendelea na ziara yake katika
Kiwanda cha Seremala gereza Kuu Ukonga, Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji na
baadaye kuongea na Maafisa na askari Bwalo Kuu la Maafisa Ukonga.
Picha zote na Jeshi la Magereza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...