Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiongea mara baada ya kumaliza kufanya uzinduzi na ukaguzi wa mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter).  Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco). 

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amepiga marufuku Mamlaka ya Bandari (TPA) kuacha kununua maji katika magari binafsi ya kusambaza maji kwa ajili ya matumizi ya kwenye meli  na kuwataka wachukue maji kutoka mamlaka inayotambulika kisheria kufanya kazi hiyo.

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mita za malipo ya kabla(Pre Paid meter) au mita za Luku katika Hotel ya Sea Cliff, Kiwanda cha Pepsi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akiwa ameambatana na Uongozi  wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasco). Akizungumza baada ya kutembelea TPA, Waziri  Mbarawa amewataka mamlaka hiyo kuhakikisha maji yote yanayotumika katika meli zinazotia nanga bandarini yanatoka Dawasco.

Mbarawa amesema kuwa matumizi ya maji yanayotoka kwa wauzaji wa nje hayajulikani yanatoka wapi na usalama wake haujilikani kwahiyo yatakapokuja kuleta madhara kwa watumiaji ndani ya meli lawama zitakuja kwa serikali na sio wauzaji hao wa maji ya maboza.

“Napenda kuwaagiza Mamlaka ya Bandari kuachana na ununuzi wa maji kutoka mamlaka zisizohusika kwahiyo Kwahiyo  masuala ya ujanja ujanja yaishe kuanzia sasa maji  na na nakuagiza mtendaji wa Dawasco ukutane na Mkurugenzi wa bandari kwa ajili ya suala hili,” amesema Mbarawa.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa amechukua maagizo hayo kama aliyovyoelekezwa na Waziri.

Dawasco wamemfunga mita hizo na zitatumika kwa wateja wakubwa pamoja na viwanda ambapo mteja atahitajika kulipia maji kabla na kiasi ulicholipia kikisha basi maji yatakatika, mfumo huo utasaidia katika kuongezea mapato Mamlaka husika pia kwa watumiaji sugu waliokuwa wanadaiwa maji kwa muda mrefu watakuwa wanalipa madeni kila watakapokuwa wananunua maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakati akikagua mfumo wa namna mfumo wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid meter) kwa wateja wa majumbani.

Mashine zilizofungwa katika kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Limited (PEPSI), kwa ajili ya wateja wa majumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...