WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bw. David Beasley
hapa nchini ni fursa itakayowawezesha Watanzania kunufaika kwa kiwango
kikubwa katika kilimo, uhifadhi na uuzaji wa mazao ya chakula
yanayolimwa hapa nchini.
Akizungumza
baada ya kukutana na Bw. Beasley jijini Dar es Salaam leo mchana
(Ijumaa, Julai 27, 2018), Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kuwa
na ziada ya chakula msimu wa mavuno utakapokamilika mwaka huu hivyo
itahitaji sana kupata soko nje ya nchi ili iweze kuuza ziada hiyo.
Taarifa
za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa mavuno ya mazao ya chakula kama
mahindi, maharage na mbaazi yatafikia tani milioni 16 wakati mahitaji ya
chakula kwa Watanzania kwa mwaka ni tani milioni 13, hivyo tutakuwa na
ziada ya tani milioni tatu,” amesema.
Akitoa
ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Julai 2018 ambapo msimu wa
mavuno bado unaoendelea, tayari nchi ina ziada ya tani milioni moja
kwani taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonyesha kuwa tayari
zimekwishavunwa tani milioni 14.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimikana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley kabla ya mazungumzo yao kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...