Na Karama Kenyunko, blogu ya JamiiMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imedai kwamba Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka ta matumizi mabaya ya madaraka ana kesi ya kujibu.
Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuleta mashahidi watano.
Hakimu Shaidi amesema amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu.Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.
Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.Miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya; mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, mwaka 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...