Na Dotto Mwaibale, Muleba

WATENDAJI wa Vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Muleba mkoani Kagera wamesema vifungashio vya dawa za serikali viliboreshwa kutoka kwenye makopo kwenda kwenye Blister pack vina uhakika wa kubakiza dawa katika ubora unaohitajika pamoja na kurahisisha kugawa dawa kwa wagonjwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mkoani Kagera, watendaji hao wamesema hata kwa upande wa watumiaji ambao ni wagonjwa vifungashio vya blister hata wakiangusha ama bahati mbaya zikamwagikiwa na maji hazitaathiriwa wala kupoteza ubora wake.

"Kupima dawa kwa kijiko kwa ajili ya kuziweka kwenye bahasha wakati wa kuwahudumia wagonjwa kulituchukulia muda sana na mara nyingine unakuta kopo linakaa wazi hadi msururu mzima unaohitaji aina hiyo ya dawa uishe"

Kwa upande mwingine wananchi wa Kata ya Nyakabango wilayani Muleba mkoani Kagera wameipongeza serikali kwa kufanikisha kuwapelekea dawa kwa wakati kupitia Bohari ya Dawa (MSD).Julius Kamuhaba alisema hivi sasa hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo ni nzuri na hakuna mtu atakayekwenda kupata matibabu akatoa malalamiko ya kukosa dawa.

"Naipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada inayoifanya ya kuhakikisha wananchi wake tunapatiwa dawa kwa wakati kupitia MSD" alisema Agnes Mganga mkazi wa kata hiyo.Alisema kila anapokwenda kupata matibabu katika Zahanati ya Nyakabango amekuwa akipata dawa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakiandikiwa kwenda kuzinunua.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Nyakabonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Fausta Rugalinda, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo pamoja na vifungashio vya dawa.
Ofisa Mauzo wa MSD Kanda ya Mwanza, Conoria Godfrey (kulia), akimuelekeza jambo Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo,Fausta Rugalinda wakati alipokuwa akikagua dawa zilizohifadhiwa kwenye stoo ya zahanati hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...