WANANCHI wameimizwa kutumia huduma za kibenki kupitia kwenye simu zao za mikononi ili kuondoa foleni kwenye benki na kujishidia zawadi mbalimbali kupitia huduma hizo.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa wiki wa promosheni ya Sim akaunti inayoendeshwa na benki ya CRDB, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Ariel Mkony, alisema kuwa huduma hiyo ya ‘Sim akaunti’ inawawezesha wananchi kujihifadhai pesa na kufanya malipo mbalimbali.

“CRDB tunaendesha promosheni kwa watumiaji wa huduma hii ambapo mshindi anaweza kupata mpaka shilingi milioni 10,” alisema Ariel.

Alisema huduma hiyo pia ni nzuri kwa watu wenye vikundi (Saccos) ambapo wanaweza wakaifadhi pesa zao na kufuatilia mihamala yote.

Aidha, katika kuchezesha droo hiyo, mkulima Lucas Kihulu wa mkoani Ruvuma aliibuka mshindi wa shilingi milioni mbili ambazo alitumiwa kwenye akaunti yake ya simu.

“Leo tumewapata washindi wawili, bwana Lucas Kihulu wa Ruvuma pamoja na Mkazi wa Mtwara, Jamal Twahili ambaye amejishindia shilingi milioni moja,” alisema Ariel.

Alisema mpaka sasa wameshatoa zawadi kwa wateja zaidi ya 400 ambao wamejisajili ya kufanya miahama la sim akaunti.
 Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa CRDB Micro Finance, Samson Keenja akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kufanyika kwa droo ya pili ya promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CRDB Micro Finance, Mikocheni jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Meneja Masoko wa CRDB Micro Finance, Ariel Mkony pamoja na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Jehud Ngolo.
 Balozi wa promosheni ya “Shinda na SimAccount”, Zuwena Mohamed (Shilolole) akizungumza wakati akiwahamasisha wana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...