BENKI ya NMB imesema itaongeza
kiwango cha mikopo inayoitoa kwa kampuni ndogo na za kati mara mbili
zaidi na kufikia Shilingi trilioni tatu kwa miaka mitatu ijayo. Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Mtengaji wa benki hiyo Bi – Ineke Bussemaker
wakati akizungumzia udhamini wa NMB kwa hafla ya Kampuni Bora 100
zamwaka 2018/2019 (Top100 Mid-sized Companies' Survey).
Kwa miaka mitatu iliyopita, NMB imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.5 kwa kampuni ndogo na za kati. Akizungumza katika uzinduzi wa utafiti wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 jijini Dar es Salaam jana, Bi. Bussemaker alisema kampuni zinazowekeza katika kufanya biashara kidigitali zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri kibiashara.
"Hatima ya uchumi wa nchi upo katika kufanya biashara kidijitali ili kuhakikisha mifumo ya utendaji inakwenda kwa kasi,” alisema na kuongeza kuwa kampuni zilizoweza kuweka mifumo sawa ya dijitali zipo katika nafasi bora zaidi ya kupata mikopo kutoka katika benki yake.
Alisema Benki ya NMB inazidi kuwekeza katika mifumo ya utoaji huduma kwa njia za kidijitali ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaohitaji huduma zake nchini kote. Kampuni Bora 100 Tanzania ni shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na KPMG.
Mbali na NMB, wadhamini wengine wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam na Azam Media na Hoteli ya Hyatt Regency.
Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...