
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) akimuonyesha Mwenyekiti wa Baraza la kilimo Tanzania (ACT) Dkt Sinare Yusuph (katikati) Barua kutoka Benki ya Kilimo inayokataa kuwapatia Mkopo wakulima wa Kijiji cha Minepa Wilayani Ifakara kwa kile walichodai mpaka wakulima hao wawe na hati miliki ya Mashamba hayo kitu kinachotajwa kuwa si sahihi, ambapo wajumbe wa bodi wameazimia kulifanyika kazi suala hilo.

Afisa Mauzo wa Kampuni ya Lonagro inayojihusisha na uuzaji wa zana za Kilimo hifadhi Bw Ray Travas akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania waliofika ofisini kwake Mjini Arusha ambapo alisema bado kuna mwitikio mdogo kwa wakulima kutumia zana za kisasa katika kilimo kutokana na uzalishaji wao kuwa mdogo huku pia wakikwamishwa na bei za mazao ambazo zimekuwa chini zaidi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafasi (TPSF) Bw. Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT),akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko na wakulima mbalimbali katika moja ya ziara ya wajumbe wa bodi ya ACT kukagua miradi inayosimamiwa na Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP).

Mkurugenzi wa kampuni ya Siza Agro Processing iliyoko Mjini Mufindi inayojishughulisha na kukoboa na kupaki kwa viwango tofauti bidhaa za mchele na unga akiwaonyesha wajumbe wa Bodi bidhaa ya Mchele inayozalishwa na Kiwanda chake, ingawa kwa sasa anasema shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho chenye mashine za kisasa unasuasua.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...