Na Mathias Canal-WK, Mufindi-Iringa


Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewataka wakulima wa Pareto kote nchini kujiunga na mfumo rasmi wa vyama vya msingi vya ushirika.

Dkt Tizeba ametoa Mwito huo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.

Alisema kuwa ushirika ni dhana ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana ambapo dhana hiyo imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. “Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya ushirika watu wengi wamekosa imani na vyama hivi na baadhi ya vyama vimeshindwa kufanya kazi vizuri hivyo nawahakikishia serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imerejesha nidhamu kwenye ushirika” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

Alisema kuwa Ushirika maana yake ni muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia wenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano.

Wanachama wa Ushirika wanaamini katika misingi ya uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine. Muundo wa Ushirika kwa ujumla unategemea uimara wa chama cha msingi cha Ushirika, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyama imara vya msingi vinaanzishwa.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua shamba la Pareto la mkulima Bahati Mhapa, katika kijiji cha Ikanga Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua kiwanda cha Pareto Mafinga (PCT) kilichopo mamlaka ya Mji wa Mafinga wakati akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...