Na.WAMJW,Bungeni,Dodoma
Idadi ya wanachama wachangiaji wa
mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708
waliokuwa wameandikishwa mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi
Septemba 2018.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye
kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini
Dodoma.
“Ongezeko hili limetokana na
kanuni na misingi inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu
ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya
mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika
usimamizi kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa kwa
upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi
Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni sawa na wanufaika wapatao
13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’ kwa hiyo mifuko hii
yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33 ya watanzania
wote kwa mujibu wa idadi ya makadirio ya watanzania kwa sasa.Idadi ya wanufaika imeongezeka
kutoka 691,774 mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa na
asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa
mpaka sasa idadi ya wanachama wengi waliojiunga asilimia 67 ni
watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema
mfuko unaendelea kutoa elimu na kubuni vifurushi mbalimbali
vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na kufaidika na mfuko ambapo
utawawezesha wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo
rasmi na kujiwekea malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.
“Mfuko umekamilisha uandaaji wa
vifurushi vya michango na mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia
bima ya afya,suala hili lipo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kwa
utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa mpango
huo utamwezesha mwananchi kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya
huduma anayoitaka kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na
wanachama watalipa kidogo kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama
‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijinini Dodoma ambapo alisema wachangiaji wa mfuko huo wameongezeka kutoka wanachama 164,706 mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 septemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa NHIF Bw.Bernad Konga akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ambapo alisema mfuko wake upo tayari kuanza mara moja kutoa huduma kupitia vifurushi vipya vitakavyojulikana kama JIPIMIE ili watanzania waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

Wakurugenzi wa NHIF wakipitia taarifa ya mfuko huo wakati ikiwasilishwa kwenye kamati mapema leo

Katibu Mkuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya(wa kwanza kulia),Mkurugenzi wa NHIF Bw.Benard Konga(anayefuata)pamoja na wakurugenzi wengine wa Wizara na NHIF wakifuatilia taarifa hiyo.

.WazirinUmmy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...