Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea miradi mbalimbali na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji  inayosimamiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya kwanza toka kuteuliwa kwake Mwamunyage ametembelea mradi wa maji wa Bunju, Mabwepande, Salasala, Wazo na Kibamba hadi Kisarawe.

Jenerali Mstaafu ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja na baadhi ya viongozi wa bodi hiyo katika kukagua miradi na  hatua iliyofikia.

Akitembelea miradi hiyo ya Maji itakayosaidia upatikanaji wa maji wa takribani Lita milioni sita kwenye Kila tanki  kwa siku, Jenerali Mstaafu Mwamunyange amefurahishwa na hatua kubwa iliyofikiwa na Dawasa katika kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya Maeneo ya Mkoa wa Pwani yanapata maji salama na ya uhakika.

Katika mradi wa Salasala unaosimamiwa na Kampuni ya Jain Irrigation Systme ambao upo katika hatua ya mwisho unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba utakaowezesha kupatikana kwa wateja wapya 40,000.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja  (wa pili Kulia) akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamjnyange (wa kwanza kushoto) wakiwa wanakagua moja ya Tanki la kuhifadhia maji wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo Leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majinsafi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian  Luhemeja  akimuelezea moja ya mradi wa maji kwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamjnyange katika ziara yake iliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa wakandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya Jain Irrigation System  wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mamlaka hiyo Leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...