Na Khadija Seif,Globu ya jamii
Balozi wa USAID nchini Marekani Inmi Petterson amepongeza juhudi za wazazi ambao wamewaruhusu watoto wao kujiunga na kupata mafunzo ya ujasiriamali na kuhitimu.
Ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuwa mustakabali wa maisha yako ni juhudi zako binafsi na si Serikali, hivyo basi waione fursa na kuifanyia kazi kwani tayari wameshapata mafunzo ya kutosha.
Petterson ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kwamba changamoto zipo na ni sehemu ya maisha na kujiamini ndio silaha tosha katika kukabiliana na maisha ili kujijengea maendeleo kwa ajili ya maslahi yako binafsi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam John Mbwana amewatangazia rasmi wahitimu hao kuwa Serikali inashirikiana mao bega kwa bega na tayari wametoa vipaumbele vya mikopo ambayo itawasaidia kufungua miradi yao wenyewe.Aidha, ameeleza wimbi kubwa linalowakuta wasichana wenye umri mdogo katika wilaya hiyo na kupelekea wingi wa vijana ambao hawana ajira nakua tegemezi kwa wazazi wao.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage Genoveva Kiliba ambayo inashughulika na kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya ujasiriamali imetoa vyeti kwa wasichana 200 jijini Dar es salaam ambao wamehitimu katika nyanja mbalimbali.Kiliba amepongeza ushirikiano ulionyeshwa baina ya wahitimu hao pamoja na familia zao ambazo zilikubali kuingia Kwenye mafunzo hayo na kuiona fursa ya kutimiza ndoto zao .
Na amesema wengi wa wasichana hao walishapoteza malengo na muelekeo wa maisha kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa mashuleni,wazazi kukosa fedha za kuendelea na masomo pamoja na vifo vya walezi au wazazi.Hivyo basi mafunzo waliyopatiwa ikiwemo elimu ya kujitambua,stadi za maisha,namna ya kufanya biashara zao itawasaidia kuendesha biashara zao kwa uweledi.
Aidha, mwalimu Makene ambae amehusika kwenye kutoa mafunzo amepongeza wasichana wote ambao wamethubutu na wameweza kunyanyuka upya na kuzikimbilia fursa hizo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...