Naibu
waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametoa wiki
moja kwa mtaalamu Elekezi wa Kampuni ya Archquants Service Limited
kuhakikisha inawasilisha michoro ya kazi za nje ya Chuo cha ufundi na
Mafunzo ya Ufundi Stadi Namtumbo kilichopo Mkoani Ruvuma ili ujenzi wa
chuo hicho uweze kukamilika.
Mheshimiwa Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho ambapo amesema ucheleweshwaji wa michoro hiyo unapelekea kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ole Nasha ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kuhakikisha wanaanzisha kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro mechanics) katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kilichopo Songea ili kupata vijana wengi watakaosomea fani hiyo.
Naibu Waziri amesema ukanda wa Nyanda za Juu Kusini unategemea sana kilimo, hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutasaidia wananchi wengi kupata uelewa wa kina kile wanachokisoma na baadae kutekeleza kwa vitendo.
“Serikali inatilia mkazo Elimu ya ufundi na imejielekeza katika kuhakikisha inapanua fursa ya vijana wengi kupata Elimu ya ufundi na ndio maana Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuweka Vyuo vya VETA katika kila Wilaya na Mkoa,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha
Naibu Waziri Ole Nasha yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa ajili ya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayasni na Teknolojia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa
ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na
baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,wakielekea
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Stadi cha
Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa
ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (katikati) na
baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua
maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha
Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akisalimiana
na baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,alipowasili
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi
Stadi cha
Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.pichani kusho
ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa
maelezo kuhusina na maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya
Ufundi Stadi cha
Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa
ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Sohia Kizigo (wa tatu kulia) na
baadhi ya viongozi waandamizi mbalimbali wa wilaya hiyo,akikagua
maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha
Namtumbo kilichopo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...