Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01
Oktoba, 2018 ameahidi kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa
ofisi ya wajasiriamali wa eneo la Feri katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es
Salaam na ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika
shughuli zao.
Mhe.
Rais Magufuli amekutana na Wajasiriamali hao ambao wanajumuisha Wavuvi Wadogo
na Mamalishe wakati akiwa katika mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama
Janeth Magufuli ambaye pia amewachangia wajasiriamali wanawake shilingi Milioni
5.
Pamoja
na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli, wajasiriamali hao wameomba awasaidie wasifukuzwe
na Manispaa ya Ilala katika eneo hilo, na badala yake wawekewe utaratibu mzuri
wa kufanya biashara zao.
Pia
wameomba waondolewe ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa
Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
kwa mitumbwi ya wavuvi wadogo wa samaki, kama ambavyo Serikali imewaondolea
ushuru wakulima wanaopeleka sokoni mazao yasiyozidi tani moja.
Aidha,
Wajasiriamali hao wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuiongoza
nchi na kushughulikia kero za Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na
kuwasikiliza kwa mara ya pili.
Kwa
upande wake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi ya Wajasiriamali
hao na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
01
Oktoba, 2018


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...