Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Jumanne tarehe 02 Oktoba, 2018 ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo jana alipokutana na wajasiriamali hao wakati akifanya mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ambaye pia ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi Milioni 5 kwa akina Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mama lishe katika eneo hilo.
Fedha hizo zimekabidhiwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kwa Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga, na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama.
Kabla ya kukabidhi fedha hizo Bw. Ngusa amesema pamoja na kutoa fedha hizo Mhe. Rais Magufuli ameagiza Manispaa ya Ilala impelekee taarifa ya mapato na matumizi ya soko la samaki la Feri haraka iwezekanavyo na amemuagiza Mkuu wa Wilaya na Manispaa ya Ilala kushughulikia kero za wavuvi na wajasiriamali wa eneo hilo ikiwemo ushuru wenye kero na tatizo la vyoo.
Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina mama wajasiriamali wa Feri Bi. Ashura Seif Nanjonga wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasaidia fedha hizo na kwa kuwajali wao pamoja na Watanzania wengine hasa wanyonge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutembelea soko la Feri na kuwasaidia wajasiriamali wa soko hilo na amesema yeye na timu yake ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wataanza mara moja kushughulikia kero za wajasiriamali hao.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto)
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam akishukuru kwa msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo PICHA NA IKULU
Habari zaidi BOFYA HAPA
Habari zaidi BOFYA HAPA







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...