Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ilikuondoa kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara jijini humo. 

Miongoni mwa mambo waliyoridhia kushirikiana ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara, usimamizi wa fedha pamoja na namna bora ya kutumia fursa ya 10% za mkopo zinazotolewa na serikali kwaajili ya vijana, Wanawake na walemavu ili fedha hizo ziwe na tija.

Aidha RC Makonda amezungumza ushiriki wa TPSF katika ziara ya Rais Dkt. John Magufuli jijini Dar es salaam ambayo tunaamini itakuwa fursa kubwa kwa sekta zote ikiwemo Biashara, uchumi, afya, elimu, miundombinu na maji ambapo amewahimiza kuitumia vizuri ziara hiyo ili kufikia ndoto ya Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara.

Pamoja na hayo RC Makonda ameelezea mpango wa kuweka kitengo cha uwekezaji (one stop center) itakayohusisha watendaji kutoka taasisi za TIC, TRA, TBS, BRELA, Uhamiaji na wadau wote wanaohusika na biashara ilikuondokana na ukiritimba uliokuwa ukipelekea mianya ya rushwa kwa wawekezaji na mwisho wa siku wawekezaji kukata tamaa ya kuwekeza Dar es salaam.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye amemuahidi ushirikiano wa kutosha kwa RC Makonda katika masuala mbalimbali yanayolenga kuliboresha jiji la Dar es salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania TPSF Bwana Godfrey Simbeye alipowasili leo na kutembelea ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...