Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imesema itachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu wa huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Onyo hilo  limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Albert Chalamila wakati akifungua mkutano wa wadau wa NHIF mkoani humo. “Kufanya udanganyifu kwa huduma za Mfuko ni kuhujumu jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kumairisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi, hivyo ndani ya Mkoa huu sitavumilia kuona hili.
 “Tunasikia kuna baadhi ya wadau wa Mfuko wasio waaminifu wamekuwa wakihujumu Mfuko huu, kwa upande wa Mkoa wa Mbeya niliweke tu wazi kuwa atakayejihusisha na udanganyifu wowote nitakula naye sahani moja, ni lazima huu Mfuko tuulinde ili uweze kuhudumia wananchi na hata vizazi vijavyo,” alisema Bw. Chalamila.
Ili kuhakikisha huduma za Mfuko zinalindwa, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wadau wote mkoani humo kuhakikisha kila mmoja anakuwa mlinzi wa huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Akisisitiza juu ya wananchi kujiunga na huduma za Mfuko, ameweka wazi kuwa ili taifa liweze kufikia malengo yake na kutimiza ndoto ya Rais Dkt. John Magufuli ya Tanzania kuwa ni nchi ya Uchumi wa Kati kupitia uwekezaji wa Viwanda ni lazima huduma za matibabu ziwe za uhakika kwa wananchi wote.
“Ni azma ya Serikali hii kuwafikia watanzania wote na huduma bora za matibabu kupitia Bima ya Afya, kukamilika kwa azma hii kutaruhusu watu wengi zaidi kutumia huduma za matibabu ambazo awali walishindwa hivyo niwaombe tu watoa huduma mjipange kuweka mazingira mazuri ya kuwahudumia watu hawa,” alisema Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Albert Chalamila akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda akihutubia wadau wa mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Beranrd Konga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko kwa Wadau wa Mkoa wa Mbeya.

 Sehemu ya Wajumbe wa Bodi ya NHIF wakifuatilia taarifa ya utekelezaji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...