Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaanza rasmi leo kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde. Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.
Mazoezi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park,MNAZI Mmoja.Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi. Madaktari ni Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya
Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa.
Kikosi kilichoitwa:
Aishi Manula (Simba)
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Frank Domayo(Azam FC)
Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC)
Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Young Africans)
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Andrew Vicent (Young Africans )
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya zaydi(Azam FC)
Kelvin Yondan (Young Africans)
Paul Ngalema (Lipuli)
Jonas Mkude (Simba)
John Boko (Simba)
Shomari Kapombe (Simba)
Feisal Salum (Young Africans)
Abdallah Kheri (Azam FC)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...