Ahmed Mahmoud Arusha

Taasisi ya mfuko wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite inatarajia kufanya Tamasha na maonyesho ya madini ya Tanzanite lengo likiwa ni kumuenzi mgunduzi wa madini hayo Mzee Jumanne Ngoma.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti mtendaji wa Taasisi hiyo Bi Asha Ngoma alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya madini mkoani hapa na kueleza kuwa katika tamasha hilo watashiriki kuonyesha zana mbalimbali alizokuwa akitumia mgunduzi huyo pamoja na madini aliyowahi kupata.

Amesema kuwa lengo la kikao kuongea na wadau kuhusu uandaaji wa tamasha la madini hayo ambapo maonyesho hayo kutangaza nchi ili madini hayo yajulikane yanatoka hapa nchini kwani sekta hiyo na wadau wake watanufaika kutokana na maonyesho hayo.

“Tunaenda kukutana na Serikali kwani wadau wamefurahia kuaandaa tamasha hili kutimiza miaka 50 tokea kugunduliwa kwa madini ya tanzanite na maonyesho hayo yatafanyika mwezi wa 12 tarehe 6-8 mwaka huu”alisema Ngoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini na vito hapa nchini(Tamida) Sammy Mollel alisema kuwa tamasha hilo limekuja wakati muafaka na kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo kwani litasaidia ukuaji wa kiuchumi na udhibiti wa madini ya Tanzanite ambapo madini haya yanatoka hapa nchini pekee amhali yalipogunduliwa madini hayo.

Amesema kuwa kutakuwa na maonyesho ya uzaji na ununuzi wa madini ya vito na pia kutembelea sehemu ambayo yaligunduliwa madini hayo ambapo tunatarajia kujenga mnara wa kuenzi ugunduzi wa madini hayo eneo hilo na tunaendelea kumpongeza mh.Rais kwa kujenga ukuta ambao unadhibiti madini hayo.

Aidha kwa upande mwingine Makamu mwenyekiti wa wafanyabiashara wa madini ya vito Tamida Thomas Munnisi alisema kuwa ni jambo jema kwa tamasha hilo kuweza kuenzi kazi nzuri ya Mzee Jumanne Ngoma na wadau wa madini ya Tanzanite wana wajibu mkubwa kuweza kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono kazi hiyo kwa kufanya Harambee kuunga mkono juhudi zake kama mh.Rais Dkt.John Magufuri alipoweza kumchangia million 100.

Alieleza jusikitishwa kwake na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo kumsahau mgunduzi hiyo Mzee jumanne ngoma kwa mchango wake kwani alitumia uwezo na rasilimali zake katika kugundua madini hayo ambayo yameweza kuwatajirisha watu wengi ilhali yeye akibakia maskini.

“Naipongeza Taasisi hii ya mgunduzi wa madini ya Tanzanite kwa uamuzi wao wa kuaandaa tamasha hilo ambalo litakuwa na maslahi mapana kwa taifa na wadau wa sekta ya madini ya vito nchini napenda kuishauri tamasha hilo likafanyika eneo la merelani ndani ya ukuta au nje ya ukuta lengo ni serikali kupata mapato yake”alisisitiza Munisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...