Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umetoa wito kwa watanzania kutmbelea Maeneo yaliyohifadhiwa hili kuweza kujionea namna Ekolojia na uhifadhi katika misitu hiyo ilivyo na faida kwa viumbe hai na Wanadamu.

akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema  jana Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog  katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam amesema kuwa watu wanpaswa kutemblea misitu hili waweze kujionea na kujifunza umuhimu wa ikolojia katika hifadhi.

"Ni vyema watu wakaja wakatembelea hifadhi ya misitu ya Amani waweze kujionea namna Misitu iliyopakana na makazi ya watu na maporoko ya maji yasikauka muda wote na kujionea maua ambayo yanaamika katika imani kuwa ndio yalitumika wakati wa kristo na watu uyafata kutoka maeneo ya mbali"amesema Mlog.

Kwa upande wakeMeneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo amewataka wadau mbalimbali kwa sasa kutembelea banda lao lililopo katika   Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kujionea huduma zitolewazo na TFS na kujua wapi wanaweza kutmebelea kwa ajili ya mapumziko yao.

Mariamu amesema kuwa Misitu inayohifadhiwa na TFS ina mambomengi sana ambayo watu wanweza kupata  ikiwa na sehemu ya kufanyia tafiti, Mapumziko kwa wana ndoa pia wanaweza kwenda kutembelea na familia zao kwa ajili ya kuwafundisha watoto umuhimu wa uhifadhi.
 Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog akizungumza na Waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo akieleza huduma za kitalii zilizopo ndani ya Hifadhi za Misitu zilizo chini ya TFS
 Afisa Misitu Mwandamizi , Anna Lawuo Akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu umuhimu wa mazao yatokanayo na misitu nchini
 Wafanyakazi wa Huduma za Misitu nchini TFS, Wakiwaonesha wadau Mazao Mbalimbali yatokanayo na misitu ambayo ni mazuri kwa ajili ya kuimarisha afya ya Mwanadamu.
Sehemu ya Mabanda ya Maonesho yakiwa yanaonekana kwa juu katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...