*Madiwani watwangana masumbwi hadharani mbele ya Polisi 
*Ni baada ya Kumbilamoto wa CCM kutangaza mshindi 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UCHAGUZI wa Naibu Meya wa Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam umeingia dosari baada ya kugeuka kuwa uwanja wa masumbwi au uwanja wa vita kutokana na baadhi ya madiwani kuamua kurushiana makonde.

Madiwani wa Manispaa ya Ilala leo walikuwa kwenye uchaguzi wa Naibu Meya baada ya aliyekuwa katika nafasi hiyo Omary Kumbilamoto kujiuzulu na kisha kujiunga CCM.

Kumbilamoto kabla ya kujiunga CCM alikuwa diwani wa CUF Kata ya Vingunguti.Hata hivyo baada ya kujiuzulu na kujiunga CCM Kumbilamoto ameshinda tena udiwani wa kata hiyo na leo amechaguliwa Naibu Meya baada ya kushinda kwa kupata kura 27 huku mpinzani wake kura 25.

Dalili za uchaguzi huo kuingia vurugu zilianza kuonekana mapema tu kutokana na kurushiana maneno kwa pande mbili ambazo zilizokuwa zinashiriki uchaguzi huo.Hata hivyo wakati wa kuhesabu hapo ndipo joto la vurugu liliposhika kasi.

Diwani wa Kata Madizini Senga kupitia Chadema aliyekuwa chumba cha kuhesabu aliamua kutoka chumba cha kuhesabu kura na kisha kupaza sauti akidai  msimamizi wa uchaguzi anaharibu uchaguzi huo.Kauli hiyo ilisababisha Polisi waliokuwa eneo hilo kuingia chumba cha kuhesabia kura kwa ajili ya kulinda usalama.

Hata hivyo wakati wanatoka chumba cha kuhesabia kura ndipo baadhi ya madiwani walianza kurushiana ngumu.Sababu za kurushiana ngumi inatokana na madiwani wa upinzani wakidai mgombea wao ameshinda kiti cha Naibu Meya lakini wanashangaa anatangaza diwani wa CCM ambaye ni Kumbilamoto.Hata hivyo Polisi walifanikiwa kutuliza vurugu hizo na hasa kudhibiti masumbwi yaliyokuwa yanarushwa kutoka kwa diwani wa upinzani kurusha makonde kwa diwani wa CCM.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo na baada ya kuhesabiwa kura hizo alimtangaza Kumbilamoto kushinda nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa hiyo.Hata hivyo madiwani wa upinzani wameonesha kutofurahishwa na matokeo ya uchaguzi huo wakidai kuna hujuma kwani wanaamini wameshinda uchaguzi huo.

Kwa kukumbusha uchaguzi wa Naibu Meya uliopita nao uligubikwa na vurugu baada ya baadhi ya madiwani walitwangana makonde ukumbini.Hata hivyo Kumbilamoto alishinda uchaguzi huo.
Baadhi ya polisi wakiwa ndani ya ukumi kutuliza vurugu zilizokuwa zimezuka wakati wa uchaguzi
Baada ya vurugu kuibuka askari waliingilia kati kuhakikisha amani inatawala kwenye uchaguzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...