SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepanga kufunza wanafunzi 200 kutoka shule sita nchini namna ya kutengeneza mfumo wa alama zinazotumiwa katika maandishi ya kompyuta na matumizi yake.
Wanafunzi hao 200 watakuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 2,489 waliofunzwa kuendeleza utaalamu wa kidijiti kwa ajili ya maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa yenye kauli mbiu “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” mafunzo yalifanyika katika shule ya sekondari ya Chazinge.Hatua hizo zimelenga kuwezesha njia ya kuelekea uchumi wa viwanda nchini Tanzania.
Pamoja na shule ya sekondari ya Chazinge na Kimani iliyopo Kisarawe mkoani Pwani nyingine ni Jamhuri, Gerezani na Benjamin Mkapa zilizopo Ilala mkoani Dar es Salaam.Katika mafunzo hayo UNESCO watahakikisha kwamba vijana wanakuwa wavumbuzi, wabunifu na hivyo kutumiwa kuboresha namna bora ya kufanya biashara miongoni mwa vijana wa kike na wakiume.
Taarifa hiyo imesema kwamba lengo kuu ni kuwezesha vijana hasa wanawake kutumia kikamilifu mifumo ya tehama kujiendeleza katika masomo ya Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM).
Alisema mafunzo hayo yataongeza pia uwezo wa vijana kujiajiri na kuajiriwa kwa kuwa na ujuzi zaidi.Mradi wa mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa UNESCO unaofanyiwa kazi katika nchi zaidi ya 25 unatambuliwa kama Youth Mobile Initiative kwa lengo la kuboresha hali za uchumi za mataifa hayo kupitia matumizi ya kompyuta.
UNESCO katika kuendeleza vijana imeshirikiana na Apps and Girls kuendesha tamasha la nne la Africa Code Week linalofanyika katika nchi 36 za Afrika tangu lianzishwe mwaka 2015.Imeelezwa katika taarifa hiyo kwamba jumla ya vijana milioni 1.8 wamefunzwa masuala ya dijiti kuelekea karne ya 21.Mafunzo hayo yamalenga kuhakikisha kwamba wanakuza uwezo wao wa kutumia alama za siri kutengeneza programu mbalimbali kwa matumizi anuai.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege akizungumza na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chanzige iliyopo wilayani Kisarawe
kuhusu nafasi ya vijana katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu
wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week”
yaliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa
yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia
Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana
shuleni hapo.
Mkufunzi
Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bw.
Wilhelm Oddo akitoa utangulizi wa elimu ya Tehama kwa baadhi ya
wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe. Haya ni moja
kati ya mafunzo ya Tehama yameandaliwa na Shirika hilo lisilo la
kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa
maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yenye lengo la
kuongeza ushiriki wa mtoto wa kike katika masomo ya Sayansi, Tehama,
Uhandisi na Mahesabu (STEM) yaliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya
miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji
Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo
mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
Wakufunzi
wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam
(kushoto) na Raymond Benedict (kulia) wakiendesha mafunzo ya Tehama kwa
vitendo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani
Kisarawe wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week”
yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa
Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili
Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo
yamefanyika jana shuleni hapo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...