Na Khadija Seif blogu ya Jamii

MCHEZAJI   video Rutyfiya Abubakari maarufu kwa jina la Amber Ruty (23), Said Bakari Mtopali (21) (kijana wake AmberRuty) na kijana anayedaiwa kuwa Shoga maarufu, James Charles Mpali a.k.a James Delicious(22) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Washtakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wamesomewa mashtaka yao leo na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Nguka Faraji.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Katuga amedai katika shtaka la kwanza linalomkabili AmberRuty peke yake, kuwa, kabla au Oktoba 25 mwaka huu katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alimruhusu mshtakiwa Mtopali kumuingilia kimwili kinyume na maumbile.
Katika shtaka la pili, mshtakiwa Mtopali anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile na AmberRuty.
Aidha, mshtakiwa Delicious anadaiwa kuchapisha na kusambaza video za kingono kupitia kompyuta kosa analodaiwa kulitenda kati au Oktoba 25, 2018 akiwa katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam.
Anadaiwa, siku hiyo alisambaza video za ngono zisizokuwa na maadili kupitia mtandao wa kijamii  wa WhatsApp
Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo wanadaiwa kati Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kwel.
Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana

Kabla ya kusomwa kwa masharti ya dhamana Wakili Katuga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za Kitaalamu kutoka kwa daktari na statement kutoka kwa mashahidi juu ya picha hizo za ngono za minato. Katika masharti ya dhamana, Mahakama imewataka washtakiwa kuwa kila mmoja kuwa na wadhamini 2 waliotakiqa kusaini bondi ya Sh. Milioni 15.
Pia wadhamini wametakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zeo za kusafiria na pia hawaruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam bila ruksa.
Hata hivyo ni mshtakiwa James Delicious pekee ndiye aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Said Bakary Mtopali wameshindwa kutimiza masharti na kupelekwa rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi November 12,2018.
 MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty) (hayupo pichani) wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.
Mshtakiwa AmberRuty wa kwanza kulia anayedaiwa kupiga naye Picha kinyume na maumbile, Said Mtopali pamoja ma James Charles maarufu kama James Delicious wakiwa nje ya chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka yao.
MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  pamoja na James Charles maarufu kama James Delicious anayedaiwa kuwa shoga wakielekea kwenye moja ya chumba cha Mahakama mara baada ya kufikishwa   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.
 MCHEZA video Rutyfiya Abubakal a.k.a Amber Ruty , Said Bakari (kijana wake AmberRuty)  wakifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yao kwa kupiga picha za utupu na kusimbaza mitandaoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...