MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo ameamua kufanya ziara katika Kata za Rwinga na Namtumbo kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.

Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.

Taarifa ya ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Mkuu wa idara ya maji alitoa majibu kwamba wanatoza 7000 flat rate kwasababu hakuna mita za maji katika baadhi ya maeneo.Hata hivyo Mkuu wa wilaya ameiagiza idara ya maji iwaandikie EWURA  kuomba kupewa mita za maji haraka ili wananchi walipe kwa haki kutokana na maji wanayoyatumia kwani sio haki kuwalipisha Sh.7000 kwa kuchota maji mara nne tu kwa mwezi tena kwa uchache.

Pia wananchi walitoa malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya huyo kuwa katika kituo cha afya Namtumbo kuna wakati dawa hawapati na 
wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa. Pia hakuna huduma za haraka kwani watendaji wa kituo cha afya wanachukua muda mrefu kuingiza taarifa kwenye komputa badala ya kuhudumia mgonjwa.

Hivyo Kizigo amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe kabla dawa hazijaisha kabisa awe ameshaagiza zingine ili ziwepo wakati wote. Lakini pia ahakikishe anaagiza dawa zinazotosha kata mbili (Rwinga na Namtumbo) kwani ni dhahiri kituo kinazidiwa na idadi ya wagonjwa kwani kinahudumia kata mbili badala ya moja.

Kuhusu matumizi ya kompyuta amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ahakikishe mafunzo kwa vitendo yanatolewa na kufanyika ili kuongeza kasi ya watumishi kuhudumia watu kwa kutumia kompyuta kwani bado hawajazizoea katika kufanya kazi zao. Pia wakati huohuo kama kuna 
mgonjwa amezidiwa waweke kipaumbele katika kumhudumia hata 
kama hawajamaliza kuingiza taarifa kwenye kompyuta.
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akizungumza na Wakazi wa Kata za Rwinga na Namtumbo,alipofanya ziara yake  kwa ajili ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kusikiliza kero za wananchi.Kizigo amefanya ziara hiyo jana ambapo amepata nafasi ya kuelezwa baadhi ya kero za idara ya maji na mazingira ya mji wa Namtumbo (NAUWASA) kutoza flat rate ya Sh.7,000 kila mwezi kwa wananchi kulipia maji, wakati maji yanatoka mara moja kwa wiki inayosababisha maji kutoka mara nne kwa mwezi.
 Wananchi wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...