NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
NAIBU Spika wa Bunge ,Dkt .Tulia Ackson amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuiga mfano wa mkoa wa Pwani ,kuvutia wawekezaji pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji ili kwenda na kasi ya ujenzi wa viwanda .
Akitembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani ,Pichandege Kibaha Mkoani Pwani ,Dkt.Tulia alisema mkoa wa huo una viwanda vikubwa 109 ambavyo ni vingi kwenye mkoa mmoja .Alieleza ,mikoa mingine ardhi zimefinywa bado hawajaona fursa hii, hivyo watenge maeneo na kuweka mipango mkakati ili kuwarahisishia wawekezaji kupata maeneo .
"Nimepita kwenye mabanda mengi ya wenye viwanda kwenye maonyesho haya ,wameonyesha nia ya kukuza viwanda vyao kwa maana ya kwamba kwenda kwenye kanda mbalimbali ,wanataka kuendeleza zoezi hili sehemu nyingine ""Tunaweza kujiiuliza kwanini viwanda vinaenda Pwani lakini kumbe wamesharahisisha kwa kutenga maeneo mengi na kujiwekea mipango na kuboresha miundombinu " alifafanua Dkt.Tulia .
Aidha ,alisema wataishauri serikali namna ya kufanya navyo kazi viwanda vya nguzo za umeme za zege kwani matumizi ya kusogeza huduma ya umeme bado ni makubwa hivyo zikitumika itasaidia tofauti na nguzo za miti ambazo zinagusa suala la athari za kimazingira .
NAIBU Spika wa Bunge ,Dkt .Tulia Ackson ,alipotembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani ,Pichandege Kibaha Mkoani Pwani (picha na Mwamvua Mwinyi)
Banda la kampuni inayojishughulisha na uingizaji wa dawa za kutibu maji nchini (Junaco), (wa katikati)ni ofisa uendeshaji wa kampuni hiyo ,Edwin Magere.(picha na Mwamvua Mwinyi)





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...