*Dola za Marekani milioni 100 kutumika katika ujenzi
*Ahimiza Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWENYEKITI
wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa amesema katika
kuhakikisha anaunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za ujenzi wa
Tanzania ya viwanda amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini
China kuja kujenga viwanda kuwekeza nchini.
Kiluwa
amesema kupitia ushawishi wake na kwa kushirikiana na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania(TIC) wawekezaji hao kutoka China wamekubali kujenga
kiwanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi, Kiwanda cha Saa pamoja
na Kiwanda cha Simu na kwamba awamu ya kwanza ya uwekezaji huo jumla ya
dola za Marekani milioni 100 zitatumika.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa wawekezaji hao Kiluwa amesema
viwanda hivyo vitajengwa Mlandizi mkoani Pwani na wakati wowote kuanzia
sasa baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo za vibali ujenzi wa
viwanda hivyo utaanza mara moja.Pia amesema mbali ya kujengwa kwa
viwanda hivyo wawakezaji hao wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha
kubangua korosho mkoani
Mtwara
na kinachoendelea sasa ni mazungumzo ambayo yanakwenda vizuri na hakuna
kitakachoshindikana."Wawekezaji hawa wameonesha nia kujenga kiwanda cha
korosho na walikuwa tayari kwenda mkoani Mtwara kuona mazingira."

Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali akizungumza jambo mbele ya waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda,ikiwemo na kuwapokea wageni wa uwekezaji wa viwanda kutoka nchini China na wenyeji wao kutoka kampuni ya Kiluwa Group Ltd.


MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa (pichani kushoto) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo alipokwenda kuwatambulisha Wadau wake wa Uwekezaji katika masuala ya Viwanda kutoka nchini China,kwa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyonayo kuhusiana na uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania,kulia ni Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akisalimia na Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group,Naima Mohamed Kiluwa,walipokwenda kwenye ofisi za kituo hicho kuwatambulisha wadau wao wa uwekezaji katika mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,anaeshuhudia pichani kati Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya uwekezaji wa viwanda hapa nchini Tanzania,maara aada kuzungumza na waandishi wa habara katika ofisi za kituo hicho .

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe walipowasili leo kwenda kutambulishwa na Mdau wake Mkubwa kwenye mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...