*Wakutwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, risasi 217,wamo Waburundi 
*Mambosasa ataja matukio ya kutisha yaliyofanywa na majambazi hayo

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema leo Novemba 29 mwaka huu maeneo ya Ubungo UFI jijini Dar es Salaam kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi kimefanikiwa kuwaua majambazi sita.

Mbali na kuua majambazi hayo wamekamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la Theophili Manirakiza mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari kuwa majambazi hao wameuawa baada ya mtego uliowekwa na askari kutokana na taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa.

Amewataja watuhumiwa hao ni Willy Irakozes maarufu kwa jina la mandoo ambaye ni wa Burundi, Jean Mugisha raia wa Burudi na Mtanzania Omary Nassoro ambaye ni Mtanzania na kwamba walikuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 8, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwaua watu sita wanaosadikika kuwa Majambazi katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo huku miongoni mwa wahalifu hao akitambulika kuwa ni raia wa kutoka nchini Burundi akiwa na kitambulisho cha Chama cha CNDD-FDD.Pichani ni kamanda wa polisi wa kanda hiyo SACP LAZARO MAMBOSASA akizungumza na wanahabari.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...