Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
Uongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) umemtangaza Mtanzania Pekee ambaye ni mwamuzi Jonesia Rukyaa kuwa amechaguliwa kuchezesha Fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana.
Rukya ni muauzi kutoka Mkoani Kagera ambaye amekuwa akiminiwa Sana katika umakini wa kazi yake na hasa katika kuchezesha mechi za Ligi kuu Tanzania bara.
Muamuzi huyo amechaguliwa katika orodha ya Waamuzi wa katikati kuchezesha michezo ya fainali za Afrika za wanawake zitakofanyika nchini Ghana.
Ambapo jumla ya Waamuzi 13 waliochaguliwa ni wa kati Kati na wasaidizi ni 12.
TFF imesema Fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazowakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zitakazofanyika mwakani nchini Ufaransa.
Ambapo Washindi Watatu wa juu ndio watakaofuzu kushiriki Kombe la Dunia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...