Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye.
Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye
Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5
Nditiye amesema kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 2.448 na kazi hiyo ilisimama kwa kipindi cha mwaka mzima mwaka 2017 na kuanza tena ambapo hadi sasa haijakamilika na imechukua kipindi cha miaka mitatu tofauti na mkataba wa awali ambapo ilitakiwa ijengwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Serikali hatuwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tunawatesa wananchi kwa kukosa huduma na kutumia vibaya fedha za Serikali,” amesema Nditiye
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati)
akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita
(hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya
Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa
fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua
wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili
kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya
Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi.
Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...