*Yaagiza mashine zichunguzwe, mitambo yenye hitilafu ikarabatiwe kazi ianze
SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.
“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.”
Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho .
Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.
Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.
“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa na wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde
wilayani Lushoto Novemba 1, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha
Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1,
2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani
Lushoto, Novemba 1, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January
Makamba, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wanne
kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Bumbuli wilayani Lushoto
akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018.
Wananchi
wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye
kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde
na kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...