Na George Binagi-GB Pazzo

Shirika la “Savings Banks Foundation for International Coorperation- SBFIC” lenye makao yake makuu nchini Ujerumani, limefungua rasmi ofisi yake nchini Tanzania lengo likiwa ni kufikisha karibu huduma zake  kwa watanzania.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo ilifanyika Novemba Mosi 2018 katika eneo la Bwiru Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, yalipo makao makuu ya shirika hilo hapa nchini huku makao makuu ya Afrika Mashariki yakiwa Kigali nchini Rwanda.

Mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini, Stephen Noel Safe alisema limejikita kuwajengea uwezo wananchi pamoja na watoa huduma za kifedha kutekeleza miradi endelevu ili kutambua umuhimu na matumizi sahihi ya mikopo pamoja na kujiwekea akiba hususani kwa taasisi ndogondogo ikiwemo Vicoba.

Mgeni rasmi, Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler kutoka nchini Ujerumani alisema huduma za shirika hilo zimewafikia wanufaika zaidi ya 2000 kwa njia mbalimbali ikiwemo mafunzo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuendeleza miradi yao kupitia huduma za kifedha ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba.


Mkurugenzi wa shirika la SBFIC hapa nchini, Stephen Noel Safe akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mtendaji Mkuu shirika la SBFIC, Dkt. Christoph Gogler akizungumza kwenye hafla hiyo.
Steven Revelian amnaye ni Mtendaji Mkuu mradi wa KARUDECA kutoka mkoani Kagera akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...