Baada ya kuwepo kwa akaunti feki ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambao ulikua unatoa taarifa mbalimbali kwa jamii kuhusu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ujumla, kuanzia leo Disemba 30, 2018, Wizara inatangaza rasmi kwa jamii, akaunti halali zilizosajiliwa kwa jina la Mheshimiwa Waziri Kangi Lugola, kama ifuatavyo; officialkangi_lugola (Instagram)
@kangi_lugola (Twitter)
Taarifa zote zitakazotolewa katika kurasa za akaunti hizi zitakua sahihi.
Kwa hatua hiyo, Wizara inaendelea kutoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha kwa kutumia jina la Kangi Lugola kusajili akaunti yoyote na kutoa taarifa za Waziri huyo kupitia akaunti feki hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Wizara inawaomba Watanzania waendelee kupata taarifa zake zaidi kupitia tovuti yenye anuani; www.moha.go.tz na twitter ya Wizara kwa akaunti ya Msemaji Mambo ya Ndani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...