Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni tatu
ili kuharakisha ukarabati wa ujenzi wa shule ya msingi Msia pamoja na
shule ya sekondari Kipeta zote za bonde la ziwa rukwa, Wilayani
Sumbawanga ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi katika kurudisha
miundombinu ya shule hizo zilizoharibika baada ya upepo na mvua kali
iliyonyehs amwanzoni mwa mwezi huu.
Kati ya fedha hizo shilingi milioni mbili zitatumika katika shule ya msingi Msia na shilingi milioni moja zitatumika kuikarabati shule ya sekondari kipeta ambapo zimebaki wiki mbili shule hizo kufunguliwa na wanafunzi kutakiwa kuendelea na masomo.
Mh. Wangabo aliwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangisha fedha kwaajili ya ukarabati wa shule ya msingi Msia zilizofikia kiasi cha shilingi 5,595,000/= ambapo wananchi wa kawaida walichangia shilingi 5000/=, wafanyabiashara wadogo shilingi 20000/=, mfangabiashara wa kati shilingi 50000/= na wafugaji shilingi 100000/= ambapo fedha hizo zinatarajiwa kufanya ukarabati na ujenzi wa madarasa manane.
Awali akisoma taarifa ya harambee ya ukarabati wa shule Mtendaji wa kijiji cha Msia Andrew Sanga alieleza mikakati ya kijiji kuwa ni kuongeza vyumba vya madarasa vitatu, na ofisi moja ya walimu na msingi umeshaaza kujengwa, kukusanya michango kwa wananchi ambao bado kuchangia na hivyo kutimiza lengo la kujenga madarasa nane, ofisi mbili ndani kabla ya shule kufunguliwa mwanzoni mwa mwezi wa kwanza.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa mapungufu yaliyopo ni kama ifuatavyo, bati, madirisha, nondo, misumari, madirisha, milango na rangi, ili kukamilisha majengo tunayoendelea kuyajenga kwani shule hiyo yenye wanafunzi 866 ina uhitaji wa madarasa 22,” Alibainisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza kushoto)akionyeshwa maendeleo ya ujenzi wa madarasa unaoendelea ili kuhakikisha shule inapofunguliwa mwezi wa kwanza wanafunzi wanapata fursa ya kuendelea na masomo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akishiriki msingi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Msia alipokwenda kuangalia ujenzi unaoendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
Kipeta Sekondari – Jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kipeta likiwa limeezuliwa paa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...