Na Dotto Mwaibale.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (Mb.) leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) ambayo mwenyekiti wake ni Dr.Fatma Mrisho. 

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni pamoja na Bi. Uphoo Swai, Dkt. Eliamini Sedoyeke, Bw. Ahmed Shaaban Kilima, Bw. Mwemezi Elnathan Ngemera, Bw. Lubengo Hilary Nyang’ula, Prof. Eligius Francis Lyamuya na Dkt. Marina Daula Njelekela ``huku mjumbe mwingine wa Bodi hiyo akitegemewa kuteuliwa hivi karibuni.

Mhe. Ummy amewataka wajumbe wa bodi hiyo, kufanya kazi kama timu moja kwa kutumia taaluma na weledi wao ili kuhakikisha wanasimamia vyema utendaji wa shughuli za Bohari ya Dawa na kufikia viwango bora vya ufanisi zaidi katika ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

Aidha amewasihi wajumbe hao kuhakikisha MSD inajiendesha kibiashara, sambamba na kuzingatia taratibu za kitaalamu zinazohusiana na usimamizi na udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na maelekezo ya sheria ya manunuzi ya umma.

Waziri Ummy ameielekeza bodi hiyo kuhakikisha Bohari ya Dawa inajiendesha vyema kifedha na shughuli zake kuendeshwa kwa gharama nafuu, kuziba mianya yote ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa aina yoyote ile, upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vyenye ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa na mwisho kusimamia, kuboresha na kudumisha matumizi ya tehama ili kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu ya Bohari ya Dawa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ` (kushoto), akimkabidhi vifaa vya kazi Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Udhamini ya Bohari ya Dawa (MSD), Dkt.Fatma Mrisho baada ya kuizindua rasmi Dar es Salaam leo.
` Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo.
Mjumbe wa bodi hiyo, Dkt.Marina Njelekela, akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa bodi.`
Baadhi ya maofisa wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...