MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.
Akizungumza DC Chongolo katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na burudani toka kwa wasanii mbalimbali, aliwataka wana-Kinondoni kuwa wazalendo kwa kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana. Alisema TTCL ni Shirika la umma na linapofanya vizuri kifaida Watanzania wenyewe ndio ufaidika tofauti na makampuni mengine yanayomilikiwa na watu wa nje ya nchi.
"...Mmesikia hivi karibuni Shirika hili lilitoa fedha shilingi bilioni moja na nusu na kuipa Serikali kama gawio, fedha hizi za Serikali hutumika kujenga miundombinu na shughuli zingine za maendeleo kwa Watanzania," alisema DC Chongolo.
Alisema kadri kampuni hii inavyofanya vizuri kifaida na jamii inanufaika hivyo kuwaomba wananchi kutumia bidhaa na huduma za TTCL Corporation ili isonge mbele zaidi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati) akionesha bango
kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani
Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL
Corporation, Bw. Ally Mbega wakishiriki. Kampeni hiyo naendeshwa na
Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza kwenye uzinduzi
rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya
hiyo usiku huu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba
akizungumza katika kampeni hizo zilizofanyika katika Uwanja wa CCM
Mwinjuma.
Msanii
Shilole akiwapagawisha washiriki katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi
Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Wasanii
Shilole na Man Fongo (kulia) wakiwapagawisha washiriki katika kampeni
ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano
Tanzania-TTCL Corporation.
Meza
kuu katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika
la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma,
wakishuhudia burudani za wasanii anuai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...