Na Linda shebby , KIBITI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji ni tulivu na salama hadi sasa hii ni kutokana na jitihada za jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na mshikamano wa wananchi.

Kamanda Lyanga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo amesema"Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote kwa kusherehekea vyema sikukuu ya Krismas mnamo Desemba 25 mwaka huu ambapo wananchi wa Rufiji walisherehekwa kwa utulivu na amani".

Aidha alisema kuwa anapenda kuwajulisha kuwa jeshi la polisi litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wadau wote ili katika sherehe za kumaliza mwaka 2018 tuendelee kuwa na usalama kwa raia wote pamoja na mali zao.

"Niwatahadharishe kuwa katika kusherehekea kila mmoja azingatie sheria za nchi kwani kuvunja sheria kwa kigezo cha furaha ya kumaliza mwaka ama kwa sababu yoyote ile ikiwemo kufanya vitendo vya kihalifu mathalani kuchoma moto matairi barabarani au mitaani , ulipuaji wa fataki, baruti, kuendesha vyombo vya moto , shughuli za disko toto na ulevi wa kupindukia havitavumilika kwani vinaweza kuwa chanzo cha madhara mbalimbali kwa binaadamu pia natoa rai kwa kila kaya kuimarisha ulinzi katika makazi yao"alisema Lyanga.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na kuimarisha ulinzi na kufanya doria na misako katika kipindi hiki cha sikukuu kwa kutumia askari waendao kwa miguu, pikipiki na magari katika miji na barabara zote kuu.

"Tunaomba wananchi mtuunge mkono kwa maslahi mapana ya taifa letu"alisema Kamanda Lyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...