Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa ajili ya mwaka mpya 2019 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na hospitali za rufaa za Temeke, Ilala na Kinondoni ikiwamo Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI). 

Zawadi hiyo imetolewa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo pamoja na wafanyakazi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza kutokana na huduma bora ambazo wanazozitoa na hivyo kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

Akizungumza katika machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa Makonda amewataka watumishi wa hospitali hizo kuongeza juhudi katika sehemu zao za kazi ili Mkoa wa Dar es Salaam uwe namba moja katika kutoa huduma mbalimbali za afya. “Idadi ya malalamiko imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za matibabu kuimarika,” amesema Makonda.

Pia, mkuu huyo wa mkoa ametoa zawadi ya ng’ombe 20 kwa Jeshi la Polisi na ng’ombe 20 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2019. Katika hatua nyingine, Makonda amesema kwamba Serikali itajenga machinjio ya kisasa na kwamba ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 8.5.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa machinjio ya Vingunguti wakati akitoa zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20 kwa wagonjwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Ocean Road, na hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam ikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana na Mwananyamala. 
Baadhi ya wananchi na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza mkuu wa mkoa kabla ya kutoa zawadi ya mwaka mpya. 
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Yacoub Hassan Mohamed akimshukuru Mh. Makonda kwa kulipatia jeshi hilo zawadi ya mwaka mpya ya ng’ombe 20. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, Mhe. Makonda na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bwana Makwaia Makani 
Mhe. Makonda akikagua ng’ombe ambao ametoa zawadi ya mwaka mpya kwa hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ). 
Baadhi ya ng’ombe wakiwa katika machinjio ya Vingunguti leo baada ya Mhe. Makonda kukabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Grace Maghembe. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...