Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akikabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi.Peter Mwaisabula walipokutana wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka.
Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhi fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme za Wizara zote kwa Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Mhandisi. Peter Mwaisabula (katikati) walipokutana wakati wa zoezi la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma leo tarehe 29 Desemba, 2018.Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Titus Mwinuka na kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo jijini Dodoma. Aliyevaa tisheti ni Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe.
Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo alipokuwa akikagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuitaka TBA kuwa na Ofisi katika eneo unapojengwa Mji wa Serikali ili kuharakisha huduma za ushauri kwa Makandarasi wanaoendelea na ujenzi wa Ofisi za Wizara mbalimbali leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji Sekta Binafsi toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bedason Shallanda.
Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma, Bw. Meshach Bandawe (kulia) akielezea jambo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu na Bunge) leo jijini Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...