NA LUSUNGU HELELA-MWANZA.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi
wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya
misitu ya Visiwa vya Kome na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa
wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.
Kauli hiyo ameitoa
wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya
Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya wavuvi wakati
alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la
Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza Naibu Waziri hiyo kuwa
kumekuwepo na changamoto ya ulipaji tozo kubwa hata kama mtu ana eneo
dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa lengo la
kupata msaada zaidi.
Amefafanua kuwa mtu
anayemiliki hekari moja anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa mwaka lakini
hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa kulipa kama wa
hekari moja kitendo kilichowafanya wananchi hao kushindwa kulipa na
kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja wa wananchi
wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba Naibu Waziri
kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya kulipa na
serikali iweze kupata mapato yake.
Kaimu Meneja wa TFS
Kanda ya Ziwa, Thomas Moshi amesema kuwa tozo hizo zipo kwa mujibu wa
sheria kinachotakiwa ni wananchi kulipa na siyo kugomea kulipa tozo hizo
na wanapofanya hivyo wanakwenda kinyume na matakwa ya sheria ya hifadhi
ya misitu.
Kanyasu
amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa
haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja kulipa tozo hizo
kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi
ili waweze kuilipa pesa hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kuwa watalipa tozo za serikali bila kulazimishwa alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Dkt. Charles Tizeba akizungumza na wananchi wa Jimboni kwake kwenye mkutano wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa kutatua kero za wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya Uvuvi iliyopo wilayani Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika kijiji cha Kisaba na Bugombe

Mwenyekiti wa Kijiji cha Buhama kata ya Buhama, Thomas Sabuni, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kabala ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ikiwa lengo kutatua kero za wananchi wa Kisiwa hicho wilaya ya Sengerama mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanya katika eneo la Kome mchangani.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu akiteta jambo na Meneja wa Shamba la Buhindi , Ayoub Kigongwira wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...