Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la Bima la Taifa Tanzania(NIC) limeshauri kwamba ufike wakati sasa kuwepo na sera ambayo itahimiza mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vita ya dawa za kulevya nchini.
Ushauri huo umetolewa leo Desemba 28,2018 na Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) Israel Severe wakati wa tamasha la Kataa Mihadarati liloandaliwa na Taasisi ya Binti Filamu chini ya Mwenyekiti wake muigzaji maarufu wa filamu Ndumbagwe Misayo a.k.a Thea .Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo alikuwa Naibu Waziri Stella Ikupa.
"Shirika la Bima la Taifa Tanzania tumeamua kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na kutambua umuhimu wake kwa jamii.Tunajua moja ya jukumu letu ni kushughulika na mambo ya bima lakini kwetu ni muhimu zaidi kuona jamii tunayoihudumia inakuwa salama kiafya.Sote tunatambua athari za matumizi ya
dawa za kulevya, hivyo tumeamua kushiriki kikamilifu kwenye vita hii ili kukomesha dawa hizo nchini.
"Tunashauri ifike wakati kuwe na sera ambayo itazungumzia umuhimu wa mashirika na taasisi mbalimbali nazo kushiriki kwenye vita hii ya dawa za kulevya.Hivyo ni wakati muafaka kwa Serikali kuweka sera itakayokwa chachu kwa mashirika na taasisi zote kushiriki kwa vitendo na iwe ni wajibu wetu,"amesema Severe.
Kuhusu tamasha hilo , Severe amesema anaupongeza uongozi wa Binti Filamu kwa uamuzi wake wa kuandaa tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wao ambao wamedhamiria kwa dhati kukomesha dawa hizo nchini kwetu.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Bw. Israel Severe ambaye ni
Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) kutokana na
mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na
tasisi ya Binti Filamu inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo
limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati Foundation jijini Dar
es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi kutokana na mchango Mamlaka hiyo katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya wakati wa tamasha la (Kataa Mihadarati Festival) lililoandaliwa na tasisi ya Binti Filamu Foundation inayoundwa na wasanii wa filamu, tamashahilo limefanyika aktika viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es salaam.
Bw. Israel Severe ambaye ni Ofisa Masoko wa Shirika la Bima la Taifa Tanzania(NIC) akizungumza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es salaam.
Kamishna wa Kitengo cha Tiba na Kinga kutoka Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...