Na Anitha Jonas, WHUSM, Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa wasanii kujitokeza na kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND.
Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Jijini Arusha alipokuwa akizindua Mfuko Mkopo wa TAGOANE LOAN FUND katika Tamasha la Tukuza Festival lililoandaliwa na Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE).
“Tumekuwa tukishuhudia wasanii wengi wenye majina makubwa wakikosa fedha hata za matibabu hili limekuwa ni suala lisilo pendeza hivyo ni vyema wasanii mkajiunga katika mfuko huu ambao utawasadia kupata mikopo yenye riba nafau na bima ya afya kupitia hili mnaweza kujikwamua kiuchumi na kujifunza kuwekeza kwa maisha ya baadae ,“alisema Mhe.Shonza.
Kwa Upande wa Rais wa TAGOANE Dkt.Godfrey Maimu alifafanua kwamba mfuko huo haubagui msanii kwani msanii yeyote anayetaka kujiunga anaruhusiwa kwani lengo la mfuko huo ni kuimarisha umoja wa wasanii na kuhakikisha maisha ya msanii yanaenda kubadilika badala ya msanii kuonekana ni mtu tegemezi na wakuomba kusaidiwa hata kwenda studio kurekodi.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
akitoa wito kwa wasanii wote nchini kujiunga na Mfuko wa Mkopo wa
TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel
Artists Network (TAGOANE) leo Jijini Arusha, alipokuwa akizindua mfuko
huo ambapo amesisitiza kuwa wasanii wa makundi yote wanaweza kujiunga.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
aliyejifunika mgorori mwekundu wa kimasai akicheza na wanakwaya wa
jamii ya Kimasai kutoka kanisa la KKKT Meserani alipowasili kuzindua
Mfuko wa Mkopo unaoratibiwa na TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) leo Jijini
Arusha.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
(aliyeketi watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) mara baada ya
kuzindua Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND) unaoratibiwa na
taasisi ya Tanzania Gospel Artists Network (TAGOANE) leo Jijini
Arusha,(aliyeketi wapili kulia) ni Rais wa Tanzania Gospel Artists
Network (TAGOANE) Dkt. Godfrey Maimu.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana
Shonza (nyuma wapili kushoto) akicheza wimbo Hapa Kazi Tu uliyokuwa
unaimbwa na Msanii Isack Chalo leo Jijini Arusha,mara baada ya uzinduzi
wa wa Mfuko wa Mkopo wa TAGOANE (TAGOANE LOAN FUND).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...