Na Dotto Mwaibale
WAZAZI nchini wametakiwa kuwa jirani na watoto wao jambo litakalosaidia kupunguza ndoa za utoto na kujiingiza katika vitendo viovu kama matumizi ya dawa za kulevya.
`Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Temeke, Faisal Hassan wakati wa hafla ya kuzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi.
" Mnajua wazazi ndio wanaochangia asilimia 70 ya watoto wao kujiingiza katika vitendo visivyofaa zikiwemo ndoa za utotoni kwa kuwa wao ndio walezi wa kwanza wa watoto hao" alisema Hassan.
Alisema katika suala la malezi ya watoto si la serikali peke yake bali ni la kila mmoja wetu hivyo uanzishwaji wa taasisi hiyo katika Kata ya Temeke ni hatua kubwa ya maendeleo pia itakuwa ni mkombozi kwa vijana kutokana na shughuli zake kujikita zaidi kusaidia vijana na kuwa Temeke ina changamoto kubwa kwa vijana kujihusisha na vitendo viovu.
Diwani
wa Kata ya Temeke,Faisal Hassan (kushoto), akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika
Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Hidaya Shomvi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Matumbi, Khatibu Lindi.
Baadhi ya watoto wanaosaidiwa na taasisi hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Msanii Hemed Mwelevu akitoa burudani wakati wa hafla ya uzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam
Bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa taasisi hiyo.
Msanii Happynes Starley, akitoa burudani wakati wa hafla ya kuzindua Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation (TAKWAFO) uliofanyika Mtaa wa Ruvuma Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...